MAAZIMIO YA MKUTANO MKUU (TAMSYA) 2016/17
BAADA
YA KUPOKEA RIPOTI, TAARIFA NA MIJADALA MBALIMBALI KUTOKA MIKOA NA MATAWI YA JUMUIYA,
MKUTANO MKUU UNAAZIMIA YAFUATAYO:
1. Tumeazimia kugawa mikoa kikanda na kupanga
waratibu kutoka kamati kuu tendaji ya Taifa watakaoshirikiana na viongozi wa
mikoa kusimamia miradi, kudhibiti upotevu wa mali za TAMSYA na kutatua migogoro
katika mikoa husika.
2. Kuanzisha na kuboresha madrasa, kambi, program za
tuisheni na somo la maarifa ya uislamu kwa shule za msingi na sekondari.
3. Kuimarisha mfumo wa upashanaji wa habari, kwa
kutoa taarifa sahihi kwa wakati ili kuboresha mahusiano mema kwa wanajumuiya na
jamii.
4. kusimamia na kutoa elimu sahihi juu ya vazi la
hijabu, kutoa miongozo na nyaraka stahiki kuhusu vazi hilo.
5. Kusimamia na kuhuisha programu za dawah
mashuleni,vyuoni kwa kushirikiana na taasisi rafiki.
VIPAUMBELE VYA MWAKA 2017.
i.
Kusajili
wanajumuiya na vikundi ndani ya jumuiya.
ii.
Kuboresha
mahusiano ya kimkakati na jumuiya, asasi za kiraia na serikali.
iii.
Kujihusisha
kwa kina katika mipango ya kuhuisha jumuiya ambayo ni:
ü
Kufanya
kambi maalumu za wanajumuiya.
ü
Kufanya
kambi za viongozi.
ü
Semina
na warsha kwa viongozi kuwajengea uwezo.
ü
Kujihusisha
na utoaji wa ushauri na nasaha kwa wanajumuiya.
iv.
Kufanya
ziara za ndani na nje ya ofisi.
ü
Ziara
za matawini.
ü
Ziara
katika ofisi mbalimbali.
ü
Kutembeleana
katika program za makaribisho na kuwaaga wanajumuiya.
v.
Kuboresha
mahusiano mema na jamii.
ü
Kutembelea
na kutoa huduma kwa wagonjwa.
ü
Vituo
vya kulelela watoto yatima.
ü
Magereza
na kutembelea wafungwa.
ü
Kutoa
hotuba na da’awa misikitini na vituo vya kiislamu.
ü
Kujitolea
kutoa damu salama kwa wagonjwa.
ü
Kutembelea
vituo vya wazee.
ü
Kupanda
miti pamoja na kufanya usafi maeneo mbalimbali ya kijamii.
vi)Kuboresha na
kusimamia utekelezaji wa majukumu ya idara ya wanawake.
0 comments:
Post a Comment