Kwa waliopata matokeo mabaya form 4, nini kifanyike!!?



WALIOPATA MATOKEO MABAYA KIDATO CHA IV 2017 

TAMSYA inasema "Hakuna sababu ya kukaa nyumbani bila ya kuendelea na masomo kwa kisingizio cha matokeo. Yeyote kwa matokeo yoyote anaweza kuendelea kusoma."

Soma makala hii, na sambaza kwa wengine ili wanufaike.

Nini cha kufanya !!?

Kabla sijamwambia nini cha kufanya ningependa kwanza kuwarudisha kwenye mstari wale waliokata tamaa kwa kupata matokeo mabaya 

Ningependa kuwashauri wadogo zangu katika kipindi ambacho baadhi yenu mmetoka kufurahi ama kusononeka baada ya matokeo ya kidato cha nne kutangazwa 

Namuomba Mungu ajalie kuwa ushauri wangu uwe msaada mkubwa kwa wale ambao hawajafanya vizuri katika mtihani na kufikia hali ya kukata tamaa na pia kwa wale ambao wanafurahi kuwa wamefaulu mtihani na kwao ukawa mwanzo wa kufaulu mitihani ijayo ama kufeli mitihani ijayo 

Kumbuka kuwa furaha ya leo inaweza kuwa msingi wa furaha ya kesho na hata hivyo huzuni ya leo inaweza  kuwa mwanzo wa furaha ya kesho, hakuna huzuni ya kudumu na ndio maana hata miba inazaa maua tena ya kuvutia na yenye manukato mazuri

kwa wadogo zangu ambao matokeo yao hayakuwa mazuri msimu huu WASIKATE TAMAA, tatizo la mtu aliyefeli mtihani sio matokeo aliyopata ila ni mtazamo wa matokeo aliyoyapata Matokeo ya mtihani wa mwisho hayatofautiani sana na matokeo ya anayopata mkulima. Mkulima akipata hasara hajutii ni kwa nini aliingia katika kilimo ila anakaa na kutafakari changamoto zilizoleta kupata hasara

Mfano huo wa maua kuota kwenye miba unatufundisha kuwa hata katika hali ya kukata tamaa kuna matumaini yanaweza kutokeza. Unapopata matokeo yasiyoridhisha, usikate tamaa, kaa tafakari, utaona njia, japo inaweza kuwa ndogo, mara nyingi njia ndogo huungana na njia kubwa mbele, ifuate tu na ndipo utaona inatanuka na kuwa kubwa

Watu wengine wanauzoefu wa kupita pasipo na njia, wao huwa wa kwanza na ndipo wengine huiona njia kwa kufuata miguu yao. Ukianzisha njia, siku unaporudi utashangaa kuona na wengine wameipita na mwisho inakuwa njia ya kudumu kwa wengi.

Nini kifanyike

Kupata matokeo mabaya katika mtihani sio lazima liwe  kosa lako, kimsingi yapo mambo mengi yanayosababisha matokeo hasi, moja ni mwalimu kwa maana ya muandaaji, pili ni mwanafunzi husika na tatu ni mazingira na miundombinu ya kujifunzia, nne sera na usimamizi wake na siasa kuziingiza kwenye elimu 

Wakati mwingine inawezekana vyote vikawa vizuri kwa maana ya kwamba mwanafunzi ni bora, mwalimu ni bora, mazingira ni wezeshi nk lakini bado matokeo yakawa mabaya

Hapo kuna jambo la kuelekeza kuhusu kwa nini bado mwanafunzi anafeli, lakini sitazungumza kwa sasa kwa vile inaweza isibadili matokeo, jambo la msingi ni kufikiri nini kifanyike

Kwa mwanafunzi aliyekuwa anajituma lakini bado akafeli, hana tofauti na mkiambiaji wa mbio za marathon ambaye amepata ajali akaanguka, je aendelee kulala pale chini kwa sababu wengine wamempita? nani ajuaye kwamba wale waliombele pia wanaweza kuanguka na kisha  wakapitwa? Na je mashindano yana mshindi mmoja tu?

Kufeli mtihani sio kufeli maisha na kama ingekuwa hivyo tungeona watu wengi walioshindwa mtihani wa shule wakishindwa kabisa maisha na pengine waliopata sifuri wakifariki dunia muda mchache baada ya matokeo 

Kwa kawaida mambo hayako hivyo na huwa yanabadilika sana, jambo la msingi ni kujipanga upya, using’ang’anie sana kuuliza kwanini imekuwa hivyo, pengine ni vema ungeuliza nifanye nini sasa hapo Mungu anaweza kukupa jibu kupitia ushauri wa watu wengine au hata wewe mwenyewe  kujiongeza

Dunia ina  fursa nyingi. Kuna fursa nyingi sana duniani ambazo ukianza kuzifanya kwa bidii utapata mafanikio na mafanikio ni mwanzo wa furaha na kufanikiwa zaidi Nakushauri kaa chini, fikiri, jipe muda, jaribu fursa nyinginezo, muombe sana Mungu, utafanikiwa tu

 Unachotakiwa usizikimbie changamoto bali zikabili kuna usemi usemao "don't limit your challenges but challenge your limits" 

Kwa wale ambao matokeo yao ni kuanzia D mbili lakini wamekosa credit tatu za kuwafanya kuendelea na kidato cha tano kuna njia zifuatazo:-
👇🏾
🔹Kuna kurudia mtihani {njia hii ngumu kidogo} 

🔹Kuna kufanya kozi za certificate {hapa inabidi uwe na D au pass zisizopungua nne} 1

🔹Kuna kufanya special certificates {hapa inatakiwa uwe na D kuanzia mbili} 

🔹Kama una zero kabisa kuna mfumo wa certificate ambazo unaziunganisha hadi unafikia malengo 

🔹Lakini pia unaweza kuendelea na kidato cha tano kwa mitihani ya UK, Cambridge na Ed excel hata kama una zero lakini hapa kuna ufafanuzi kidogo 

Haya kazi kwenu nimekupeni njia tano hizo mshindwe wenyewe tu 

Tunasubiria maswali kutoka kwenu
Andika swali lako kwenye kibox cha COMMENT hapo chini



Share on Google Plus

About UPStream Telecom

2 comments: