Maana ya Kusimamisha
Swala.
Ni kuswali kwa
kutekeleza kikamilifu nguzo, sharti zote za swala na kuwa na unyenyekevu
(khushui) ndani ya swala.
Nafasi na Umuhimu wa
Kusimamisha Swala katika Uislamu.
Swala imesisitizwa na
ina umuhimu katika Uislamu kwa sababu zifuatazo;
i.
Kusimamisha Swala ni Amri ya Mwenyezi Mungu (s.w).
Mwenyezi Mungu (s.w) ameamrisha waumini
(waislamu) wote wasimamishe swala zote za faradh na sunnah ipasavyo.
Rejea Qur’an (29:45), (4:103) na
(14:31).
ii. Kusimamisha swala ni nguzo ya Pili ya Uislamu.
Baada
ya shahada mbili, nguzo ya pili na ya msingi mno katika Uislamu ni kusimamisha
swala.
iii. Swala humtakasa muislamu na mambo machafu na
maovu.
Bila shaka swala ikiswaliwa vilivyo humuepusha mja na mambo machafu na
maovu.
Rejea Qur’an (29:45).
iv. Swala ni amali ya mwanzo kabisa kuhesabiwa siku
ya Qiyama.
Swala ya muumini ikitengemaa vizuri ndio sababu ya kufaulu kwake Duniani
na Akhera pia.
Rejea Qur’an (23:1-2,9), (87:14-15)
na (22:34-35).
v. Kutosimamisha swala ni sababu ya mtu kuingizwa
motoni.
Hii ni baada ya muislamu Kupuuza swala kwa
kutozingatia sharti na nguzo zake kikamilifu na kukosa unyenyekevu (khushui)
ndani ya swala.
Rejea Qur’an (74:42-47), (68:42-43) na
(107:4-5).
Lengo la Kusimamisha
Swala.
Lengo kuu la kusimamisha
swala ni kumkinga mja na mambo machafu na maovu kwa kutekeleza kikamilifu
sharti, nguzo na sunnah za swala pamoja na kuwa na khushui ndani ya
swala kama ifuatavyo;
i.
Swala inamtakasa mja kwa
kuzingatia na kutekeleza sharti zake zote kikamilifu ambazo ni kuwa twahara,
sitara (kujisitiri), kuchunga wakati wa swala na kuelekea Qibla.
ii.
Swala inamtakasa mja kwa
kutekeleza kikamilifu nguzo na sunnah za swala kama kumsifu na
kumtukuza Mwenyezi Mungu (s.w), kusoma Qur’an, kutoa ahadi ya kujisalimisha kwa
Mwenyezi Mungu (s.w), kuomba dua na kutekeleza vitendo vyote vya swala.
0 comments:
Post a Comment