MASWALI NA MAJIBU
SWALI LA (1)
Mtu anasali nyuma imamu lakini anaenda nae sambamba imamu wake katika kuhama Vitendo au akawa anamtangulia ipi sawa?
MAJIBU :
Ni makosa makubwa kwenda na imamu sambamba katika vitendo bali unafaa usubiri mpaka atangulie, makosa mengine pia Haifai kumtangulia imamu na Ukintamgulia IMAMU SALA INABATILIKA
📚DALILI
عَنْ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ رَكِبَ فَرَسًا فَصُرِعَ عَنْهُ فَجُحِشَ شِقُّهُ الْأَيْمَنُ فَصَلَّى صَلَاةً مِنْ الصَّلَوَاتِ وَهُوَ قَاعِدٌ فَصَلَّيْنَا وَرَاءَهُ قُعُودًا فَلَمَّا انْصَرَفَ قَالَ إِنَّمَا جُعِلَ الْإِمَامُ لِيُؤْتَمَّ بِهِ فَإِذَا صَلَّى قَائِمًا فَصَلُّوا قِيَامًا فَإِذَا رَكَعَ فَارْكَعُوا وَإِذَا رَفَعَ فَارْفَعُوا وَإِذَا قَالَ سَمِعَ اللَّهُ لِمَنْ حَمِدَهُ فَقُولُوا رَبَّنَا وَلَكَ الْحَمْدُ وَإِذَا صَلَّى قَائِمًا فَصَلُّوا قِيَامًا وَإِذَا صَلَّى جَالِسًا فَصَلُّوا جُلُوسًا أَجْمَعُونَ
Imepokewa na Anas ibn Malik kuwa Mtume wa Allah ((Swalla allahu alayh wasalam)) alikuwa akimwendesha farasi na kisha akaanguka upande wa kulia wa Ubavu wake na akapata majeraha
kisha akasalisha amekaa kisha baada ya sala yake akasema
((Imamu amewekwa ili afuatwe ikiwa amesali amesimama sali nae huku umesimama, akirukuu pia nawe Rukuu ,akiitidali pia nawe itidali akisema "SAMIAH ALLAHU LIMAN HAMIDAH" semeni "RABBANAH WALAKAL HAMDU"))
akisali huku amesimama salini nae huku mmesimama ,akisali amekaa basi pia salini nae huku mmekaa!!
_____
Bukhaary - hadith ya 648
" رواه البخاري-648
Faida nyingine Katika Hadith hii
✔ Ikiwa Imamu wenu anayewasalisha hawezi kusali kasimama kwa maradhi basi yajuzu kusali mkiwa katika hali yake ya kukaa kwa DALILI hii na zingine ambazo zimethibiti.
0 comments:
Post a Comment