Swali namba 2

MASWALI NA MAJIBU

SWALI LA (2)

Inasomwa Dua ya Qunuut wakati wa Witr baada ya Tarawehe kukawa  na Baadhi ya Watu wanaitikia Dua huku Wamenyanyua Nyuso zao Mbinguni....kufanya hivi ni sawa?

MAJIBU:

Sio Sawa na Imekatazwa kwa Katazo kali sana na Mtume ((Swalla allahu alayh wasalam)

inatakiwa Mtu aitikie Dua huku kaelekea Mahala pake pa sujuud inatosha

📚DALILI YA KATAZO

ما روى البخاري (750)

Imepokewa na Imam Bukhaari


 عن أَنَس بْن مَالِكٍ رضي الله عنه قَالَ : قَالَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ :

Anas Ibn Malik ((Allah amuwie Radhi)) alisema

Mtume ((Swalla allahu alayh wasalam)) Alisema


( مَا بَالُ أَقْوَامٍ يَرْفَعُونَ أَبْصَارَهُمْ إِلَى السَّمَاءِ فِي صَلَاتِهِمْ فَاشْتَدَّ قَوْلُهُ فِي ذَلِكَ حَتَّى قَالَ : لَيَنْتَهُنَّ عَنْ ذَلِكَ أَوْ لَتُخْطَفَنَّ أَبْصَارُهُمْ )

((Wana matatizo gani watu ambao wananyanyua nyuso zao mbinguni ndani ya sala?))

Aliongea kwa Ukali sana mpaka akasema

((Waache jambo hili au ama laah Wataondolewa Kuona kwao (watatiwa Upofu))
Share on Google Plus

About UPStream Telecom

0 comments:

Post a Comment